Imeandikwa na kukaguliwa na madaktari wa Developing Medicine wanaozungumza Kiswahili
Ilikaguliwa mwisho: 16 Novemba 2026 · Ukaguzi unaofuata: 16 Novemba 2027
Madaktari wetu wanajadili njia nne rahisi za kupunguza shinikizo la damu.
Shinikizo la damu la juu wakati mwingine huitwa “muuaji wa kimya”. Kwa kawaida halina dalili, lakini kwa muda huharibu macho, moyo na figo. Watu wengi wanaopata mshtuko wa moyo pia wana shinikizo la juu la damu.
Kipimo cha kawaida ni karibu 120/80. Kipimo cha 130/90 au zaidi ni cha juu. Ukiambiwa una shinikizo la juu la damu, usilipuuze. Muulize mhudumu wa afya kama unahitaji pia dawa.
Kama shinikizo linabaki juu licha ya mabadiliko haya na dawa, muone mhudumu wa afya.
Muhimu: Taarifa hii ni kwa ajili ya elimu ya jumla. Haichukui nafasi ya ushauri wa mhudumu wa afya. Ikiwa una wasiwasi kuhusu afya yako, au dalili zako zinazidi kuwa mbaya, muone mhudumu wa afya. Katika dharura, nenda mara moja kwenye kituo cha afya kilicho karibu nawe.
Madaktari wetu huandika na kukagua kila nyenzo. Jinsi tunavyotayarisha nyenzo zetu
Ukiona kosa, tafadhali tutumie barua pepe: doctors@developingmedicine.org

Cookie compliance notice: We use cookies to optimise your experience on this website and to understand how it is being used. Feel free to deny or manage these cookies. More information can be found in our Privacy and Cookies Policy.